Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#CAFCC: Singida FG yapewa JKU ya Zanzibar

Singida Jezi Singida FG yapewa JKU ya Zanzibar

Tue, 25 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Singida Fountain Gate itakutana na JKU ya Zanzibar katika hatua ya kwanza ya michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika na mshindi kati ya timu hizo atacheza na Future SC (Misri) katika raundi ya pili.

Michezo ya raundi ya kwanza itapigwa kati ya Agosti 18, 19 na 20, mwaka 2023 na marudiano yatakuwa Agosti 25, 26 na 27 wakati raundi ya pili itachezwa Septemba 15, 16 na 17 na marudiano yatakuwa Agosti 29, 30 na Oktoba 1, 2023.

Baada ya kutamatika kwa raundi ya pili, mshindi wa Jumla atafuzu hatua ya Makundi ya Kombe ya Shirikisho Afrika.

Future FC imemaliza nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu ya Misri ikiwa imecheza michezo yote 34, alama 58, kushinda mechi 15, kufungwa mechi 6, sare 13, mabao ya kufunga 34 na mabao ya kufungwa 23.

Aidha, Singida FG ataanzia nyumbani katika mchezo huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live