Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CAFCC: Simba kukutana na Uhamiaji ama Bingwa wa FA Libya

Simba Sc Usajili CAFCC: Simba kukutana na Uhamiaji ama Bingwa wa FA Libya

Thu, 11 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika droo ya Kombe la Shirikisho Afrika, Klabu ya Simba ambayo itaanzia hatua ya pili ya mtoano, imepangwa kucheza na mshindi kati ya Uhamiaji ya Zanzibar na Bingwa wa FA nchini Libya.

Coastal Union ambao wataanzia hatua ya kwanza ya mtoano, wao watacheza dhidi ya FC Bravo ya Angola na atakayefuzu atakipiga dhidi ya Fc Lupopo.

Mechi za mkondo wa kwanza wa hatua ya awali zitapigwa kati ya Agosti 16 - 18 huku marudiano yakitarajiwa kupigwa kati ya Agosti 22 - 25, 2024.

Mechi mkondo wa kwanza wa raundi ya kwanza zitapigwa kati ya Septemba 13-15, 2024 huku marudiano yakitarajiwa kupigwa kati ya Septemba 20-22, 2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live