Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#CAFCC: Azam FC mdomoni mwa Club Africain

Sad Azam Azam FC mdomoni mwa Club Africain

Tue, 25 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Soka ya Azam FC imepangwa kumenyana na Bahir Dar Kenema FC ya Ethiopia katika Raundi ya Kwanza ya Mchujo ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) na mshindi atacheza na Club Africain (Tunisia) katika raundi ya pili.

Mchezo wa awali utafanyika kati ya Agosti 18 hadi 20, 2023 ugenini kabla ya mechi ya marudiano kupigwa kati ya Agosti 25 hadi 27, Azam Complex.

Raundi ya pili michezo itapigwa kati ya Septemba 15, 16 na 17 na marudiano yatakuwa Agosti 29, 30 na Oktoba 1, 2023.

Baada ya kutamatika kwa raundi ya pili, mshindi wa Jumla atafuzu hatua ya Makundi ya Kombe ya Shirikisho Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live