Dakika chache kabla ya timu kuingia kupasha misuli Yanga imejikuta katika presha baada ya Afisa wa Shirikisho la Soka Afrika CAF kuzuia mipira ya timu wenyeji.
Iko hivi wakati mashabiki wakisubiri timu zao kuja kupasha misuli huku kila timu ikiwa imepanga vifaa vyake vya mazoezi Hosameldien Elzanaty ambaye ni mratibu wa mchezo alimuita mtunza vifaa wa Yanga na kumtaka kuondoa mipira yao uwanjani.
Baada ya kukabidhiwa mipira hiyo hiyo ili aondoke nayo na kurudi nayo vyumbani ambapo dakika tatu baadaye wenyeji Yanga waliingia uwanjani kuja kupasha misuli.
Hata hivyo haraka kocha wa viungo wa Yanga Helmy Gueldich alipoambiwa mipira yao imechukuliwa alirudi vyumbani haraka kisha akarudi na mipira hiyo huku akiongea na Elzanaty.
Baada ya mazungumzo yao Elzanaty alichukua mipira hiyo mitano na kuwapa wageni TP Mazembe huku mingine ilibaki kwa Yanga.
Mazembe kabla ya hapo walikuwa na mipira saba pekee uwanjani na baada ya uamuzi huo wakawa na jumla ya mipira 12 sawa na Yanga.
Tayari timu zote zinaendelea na mazoezi uwanjani kuelekea mchezo wa wa pili kwa timu zote wa Hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.