Shirikisho la mpira wa miguu Afrika (CAF) imetoa pongezi kwa timu ambazo zimekamilisha vigezo vya kupata leseni za klabu ambazo zitacheza mashindano ya kimataifa.
Miongoni mwa klabu zilizopatiwa leseni na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ni, Yanga na Simba zinazocheza Ligi ya Mabingwa, na Azam Fc na Singida Big Stars zinazocheza kombe la Shirikisho baada ya kukidhi vigezo.
CAF imeendelea kuzikumbusha klabu hizo kuwa kwa mujibu wa kanuni yake ya leseni za klabu ya 2022, zinatakiwa kutekeleza vigezo na masharti yote ya kanuni hiyo ya msimu mzima, na ikitokea zimekiuka, leseni hizo zitafutwa.