Mabosi wa Azam na Singida Big Stars hawana namna tena baada ya kutaitiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuagiza kwa klabu zote zilizokata tiketi ya michuano ya kimataifa kwa msimu ujao, kulazimika kuwa na timu ya soka ya wanawake kama moja ya vigezo za kushiriki michuano hiyo.
Timu hizo sambamba na Yanga na Simba ndizo zitakazoiwakilisha nchi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho baada ya zote kumaliza ndani ya nne Bora, Yanga ikitwaa ubingwa, Simba ikimaliza nafasi ya pili na Azam na Singida zikifuata nyuma ya vigogo hao.
Kwa mujibu wa kanuni mpya za CAF, klabu yoyote itakayoshiriki michuano ya kimataifa itatakiwa kuwa na timu ya wanawake au kuingia makubaliano na timu ya wanawake, ambapo kwa Simba na Yanga wala sio ishu sana kwa vile tayari zina timu hizo, Simba Queens na Yanga Princess.
Hata hivyo, kutokana na kiu ya kushiriki michuano hiyo, Azam na Singida zitazoshiriki Kombe la Shirikisho zimeanza mchakato huo ili kuwahi siku ya mwisho ya uwasilishaji wa timu hizo ambao ni Juni 30, ikiwa na maana ya wiki tatu zijazo tu. Ofisa Habari wa Singida Big Stars, Hussein Masanza amesema kwa sasa wanakamilisha ratiba ya michezo ya Ligi Kuu, lakini muda wowote watatambulisha timu ya wanawake.
Masanza alisema tayari viongozi wa timu hiyo washamaliza taratibu zote hivyo kabla ya Juni 30 wataweka bayana kwani kila kitu kinafanyika kwa sasa kimyakimya.
"Tunasubiri tumalize mchezo mmoja wa ligi na kusubiri usiku wa tuzo za TFF rasmi tutaitambulisha timu ya Singida ya wanawake, kwani hatuwezi kuipoteza nafasi ya kwenda CAF," alisema Masanza, huku Mkuu wa Kitengo cha Habari, Thabiti Zakaria 'Zaka Zakazi' alisema wao watachagua sheria ya pili kuingia makubaliano na timu mojawapo ya wanawake ili kupata kibali cha kushiriki CAF.
"Najua hakuna timu itakayokataa kuingia makubaliano na timu yetu kwa sababu inafanya vizuri Ligi Kuu tupo kwenye mchakato huo ikiwa tayari tutawaambia," alisema Zakazi.
Singida hii itakuwa michuano ya kwanza ya kimataifa kwao, ilihakli Azam itakuwa ni msimu wa nane kwani msimu huu ilitolewa raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho kwa kutolewa na Al Akhdar ya Libya kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya kufungwa ugenini 3-0 na kushinda nyumbani