Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CAF yampasua kichwa Nabi

Nabi X Kaze Ahadi CAF yampasua kichwa Nabi

Tue, 3 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, amefichua kuwa, licha ya ushiriki wao katika Kombe la Mapinduzi, lakini mipango na mikakati yake mikubwa ipo kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, michuano inayosimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), kwa kuwa wanataka kufanya makubwa.

Nabi ametoa kauli hiyo kabla Yanga kucheza mchezo wa kwanza wa Kombe la Mapinduzi Kundi B dhidi ya KMKM, kesho Jumatano.

Katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi, Yanga imepangwa Kundi D na timu za US Monastir ya Tunisia, Real Bamako (Mali) na TP Mazembe (DR Congo).

Kocha huyo ameliambia Spoti Xtra kwamba: “Hatuna sababu ya kupuuza wala kukwepa kwa sababu ni mashindano ambayo yapo karibu kila mwaka na lazima tushiriki kwa ajili ya kutafuta ubingwa kama ilivyokuwa katika misimu mengine kwa sababu ni heshima kwetu kuchukua ubingwa wa michuano hii.

“Lakini binafsi nimekuwa nikiangalia zaidi Kombe la Shirikisho Afrika kwa sababu tunahitaji kufanya vizuri na kufika katika hatua kubwa kutokana na wapinzani ambao tutakutana nao, ukiangalia TP Mazembe, Real Bamako na hata Monastir wote siyo wa kupuuza.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live