Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CAF yamgomea Saido Simba Sc

Saidoo Simba CAF yamgomea Saido Simba Sc

Thu, 5 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo fundi wa Simba, Said Ntibazonkiza ‘Saido’ amefunguka sababu za kuvaa jezi namba 39 na kusema kuwa CAF waliigomea namba aliyokuwa anaitaka awali.

Saido ambaye amezoeleka kuvaa jezi namba 10, amesema baada ya kubaini kuwa jezi hiyo tayari ina mtu ndani ya kikosi cha Simba ambaye ni Pape Sakho, aliuomba uongozi umruhusu kuvaa namba 60 lakini ilikuwa ngumu.

Iko hivi; Simba ambao wanaiwakilisha nchi kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika wamemwambia staa huyo kuwa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), haliruhusu mchezaji anayeshiriki mashindano hayo kuvaa jezi yenye namba zaidi ya 40.

Ndipo nyota huyo alipoamua kuishirikisha familia yake ambayo iliamua kumchagulia namba 39, ambayo alishawahi kuivaa nje ya Tanzania.

“Nina namba zangu huwa napenda kuzivaa ambazo ni 10, 26, 39 na 60, baada ya kuona Simba namba yangu pendwa ina mtu sikutaka mambo mengi nikachagua 60, lakini kikanuni CAF hairuhusiwi,” alisema.

“Ndipo nilipoamua kuishirikisha familia yangu, watoto wangu wakaamua kuchagua namba 39, ambayo pia kwenye rekodi zangu nje ya Tanzania imenifanyia makubwa.”

Saido ambaye amesajiliwa na Simba dirisha hili la usajili tayari ameonyesha umuhimu wake ndani ya timu hiyo, akifunga mabao matatu na asisti moja ndani ya timu hiyo.

“Nawaomba mashabiki wa wetu wawe na subra mpira wa miguu una matokeo matatu kuna nyakati za furaha na huzuni wasituache tunawategemea sana tutaendelea kuwapa furaha.

“Nimefurahia namna walivyonipokea ndani ya timu yao nawaahidi kuendele kuwapa furaha kadiri nitakavyokuwa napata muda wa kucheza ndani ya timu nitakuwa mchezaji mwenye kutoa ushirikiano kwa wenzangu na benchi la ufundi.” alisema supataa huyo wa zamani wa Yanga aliyeondoka Jangwani msimu uliopita akiwa na rekodi tamu katika Ligi Kuu Bara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live