Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CAF yaimpa jeuri Robertinho

Robertinho Hgs.jpeg CAF yaimpa jeuri Robertinho

Fri, 26 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Simba, umemuhakikishia kocha mkuu wa timu hiyo, Mbrazil, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ wataweza kumsajili mchezaji yeyote atakayemtaka kuelekea katika msimu ujao kutokana fungu kubwa la fedha wanazotarajia kupewa na Shirikisho la Soka Afrika ‘CAF’.

Simba inatarajia kuvuna fedha kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF) zikiwa ni maandalizi ya Super League lakini pamoja na zile za hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu, ambazo ni ni Dola 900,000 (zaidi ya Sh 2.1 Bilioni).

Akizungumza nasi, Mkuu wa Idara Habari na Mawasiliano ya Simba, Ahmed Ally alisema kwa fedha wanazozipata kutoka CAF ikiwemo Super League na vyanzo vyao vingine vya fedha ikiwemo kwa mwekezaji wao Mohammed Dewji (Mo Dewji) zitawasaidia kumchukua mchezaji yoyote atakayehitajika ndani ya kikosi hicho.

“Tumekuwa na mzigo mkubwa ikiunganisha fedha za mwekezaji wetu, Mohammed Dewji, vyanzo vya Simba pamoja na fedha za Super League hali hiyo tutafanya usajili mkubwa na tunaweza kununua klabu 15 za hapa ndani na hii inamanisha tunapokea mzigo mkubwa.

“Tuko katika mawindo makali tunaangalia watu kadha wa kadha ndani na nje ya Tanzania, Bajana tunamkubalia sana ni kijana ambaye ni mzuri, kocha Robertinho (Roberto Oliveira) akipendekeza basi tutafanya mazungumzo na Azam kupata huduma yake,” alisema Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: