Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CAF yailainishia Yanga

Yanga Vs Augusburg CAF yailainishia Yanga

Thu, 18 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika kundi la timu sita za Tanzania zitakazo wakilisha Kimataifa msimu huu, upepo unaonekana kuiendea vizuri Yanga baada ya kupata taarifa kuwa wapinzani wao Vital’O ya Burundi haitotumia Uwanja wao wa nyumbani wa Intwali kwa mechi za nyumbani kutokana na uwanja huo kutokidhi vigezo.

Timu za Burundi zimekuwa zikitumia viwanja vya Benjamin Mkapa na Azam Complex vilivyopo Dar es Salaam, Tanzania kwa mechi zao za nyumbani jambo linaloweza kuwa la neema kwa Yanga ikiwa Vital’O wataamua kucheza mechi yao ya nyumbani wakiwa Tanzania.

Lakini Yanga ikipenya na kuingia hatua inayofuata, inaweza tena kupata neema ya kutocheza katika nchi husika ambayo mpinzani wake anatokea ikiwa wawakilishi wa Ethiopia, CBE watafuzu mbele ya SC Villa ya Uganda.

Ethiopia haina uwanja ambao utatumika kwa mechi za hatua za mwanzo za mashindano ya klabu Afrika kwa vile Caf haikupitisha viwanja vyake baada ya kukosa sifa ya kutumika kwa mechi za mashindano hayo. Hilo linailazimu CBE na timu nyingine ya Ethiopia inayoshiriki Kombe la Shirikisho Afrika kucheza mechi zao za nyumbani katika viwanja vya nchi nyingine.

Bahati nyingine kwa Yanga ni kukosekana kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa baadhi ya timu ambazo zimeizidi pointi katika viwango vya ubora wa Caf, jambo ambalo litaifanya Yanga ipangwe katika chungu cha pili kwenye upangaji wa droo ya hatua ya makundi ikiwa itafanikiwa kuingia hatua hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: