Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CAF yaichinja Biashara United Kimataifa

Biasharautd 241182653 2985254285074728 9199527890377565480 N?fit=800%2C525&ssl=1 Kikosi cha Biashara United

Wed, 3 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ya Matumaini tuliokuwa nayo awali hatimaye Klabu ya Biashara United imetolewa rasmi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kushindwa kusafiri kwenye mchezo wa marudiano dhidi ya Al Ahly Tripoli ya Libya.

Katika barua iliyotumwa na CAF kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeeleza kuwa uamuzi wa kuiondosha timu hiyo umefanywa na kamati ya mashindano ya Shirikisho hilo.

Kwa mujibu wa CAF wameeleza kuwa sababu zilizoifanya timu hiyo kushindwa kwenda Libya kucheza mechi hiyo ya hatua ya pili ya raundi ya awali hazikutokana na dharura za mechi hiyo ambayo ilipangwa kufanyika Oktoba 23, Jijini Benghazi nchini Libya.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa Oktoba 15 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa timu hiyo iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Kwa mantiki hiyo Tanzania imebaki na mwakilishi mmoja tu katika michuano ya kimataifa, ambao ni Simba SC wanaoshiriki Kombe la Shirikisho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live