Shirikisho la Soka Afrika CAF limefungia viwanja viwili vya soka huko DRC navyo ni Uwanja wa Kibassa Uwanja wa nyumbani wa St. loi Lupopo ya Lubumbashi na Uwanja wa Marty's unaotumiwa na Darling Club Motemapembe wa Kinshasa.
Uwanja pekee wenye hadhi ya kutumiwa kwenye kampeni za CAF ni Uwanja wa TP Mazembe, uliopo Lubumbashi. Raisi wa Mazembe @moisekatumbi.officiel ameweka wazi yupo tayari kuruhusu timu yoyote ya DRC kutumia Uwanja wao.
Kumbuka DRC wana timu 4 kwenye hatua ya Makundi Msimu huu, AS Vita Club Ligi ya Mabingwa, TP Mazembe, Lupopo na Motemapembe wote Shirikisho.
Lupopo ni wapinzani wa jadi na Mazembe, Wanaonekana kugomea mpango huo Wanafikiria kwenda kucheza mechi zao Zambia, AS Vita nao Wanafikiria kwenda Brazzaville Nchi jirani kucheza mechi zao.
Vita Club ipo Kinshasa ambako kutoka huko mpaka Lubumbashi ni saa 2 kwa ndege, Lakini kwenda Brazzaville ni Dakika 10 kwa Boti.