Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CAF yaanza na Yanga mchana kweupe

Yanga Lubumbashi CAF yaanza na Yanga mchana kweupe

Fri, 31 Mar 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mziki wote wa Yanga umeondoka jana Alhamisiusiku kwenda DR Congo tayari kwa mechi muhimu ya kukamilisha hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe.

Ni kati ya mechi ngumu za wikiendi hii ambazo zitatoa uelekeo wa mpinzani wa Yanga kwenye hatua ya robo fainali zilizopangwa kuanza Aprili 23 mwaka huu.

Kwa mujibu ratiba ya wikiendi hii kwenye michuano hiyo Kombe la Shirikisho, Yanga ikiwa Kundi D kuna mechi nane ngumu, lakini Caf wameitanguliza mechi ya Yanga na Mazembe ambayo itaanza saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Mazembe, jijini Lubumbashi.

Licha ya kwamba wenyeji hata wakishinda mabao 100 hawatakwenda popote, ndio mechi pekee ambayo itachezwa mchana nyingine zote zitaanza kuanzia usiku.

Mechi mbili za Kundi B zitachezwa saa 1:00 usiku ambazo zile zingine za makundi A, C na moja ya kundi D itachezwa saa 5 usiku muda huo Yanga watakuwa wametulia hotelini wakianza kutabiri nani watakayekutana nae robo.

Yanga inaombea kuongoza kundi lao ili waanzie kikanuni hawawezi kukutana na timu yoyote waliyokuwa nayo kwenye kundi moja. Hadi sasa timu ambazo zimeshafuzu moja kwa moja ni Marumo Gallants (Afrika Kusini), Rivers United (Nigeria), Monastir (Tunisia) na Asec Mimosas ya Ivory Coast na Yanga.

Yanga ikiwa na mzuka wa aina yake juzi walifanya vikao kadhaa kwenye kambi yao ya Avic katika kuwekana sawa kwa safari ya yao na kile wanachokitegemea kwenye mchezo huo, huku Kocha Nasreddine Nabi akisisitiza kwamba mkakati wao ni kushinda si vinginevyo na hawatabweteka hata kama ni mechi ya kukamilisha ratiba.

Yanga iliyotarajiwa kuondoka saa 5 asubuhi, ikiwa ndio kinara wa kundi D ikiwa na pointi 10 sawa na ilizonazo Monastir ya Tunisia ambayo yenyewe itamalizana na Real Bamako iliyopo nafasi ya tatu zikitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.

Katika mechi ya mkondo wa kwanza, Yanga iliinyoosha TP Mazembe kwa mabao 3-1 Kwa Mkapa jijini Dar es Salaam ikiwa ni rekodi tangu ianze kushiriki michuano ya CAF ilikuwa haijwahi kuifunga timu hiyo, kadhalika ni mara ya kwanza kuongoza kundi tangu iliposhiriki michuano hiyo ya Afrika.

Juzi mchana mabosi wa Yanga walikuwa wakimaliza taratibu katika Ubalozi wa DR Congo uliopo nchini, huku mastaa wa timu hiyo waliokuwa wameruhusiwa kwenda makwao kuaga ili kujiandaa na safari hiyo na mara timu itakaporudi itacheza mechi ya robo fainali ya ASFC dhidi ya Geita Gold Aprili 8 na siku mbili baadae itaumana na Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu

Taarifa kutoka ndani ya Yanga inasema kuwa Denis Nkane, Bernard Morris Dickson Ambundo na Aduutwalb Mshery, huku wachezaji waliopo kwenye timu zao za taifa wakitarajiwa kuungana na timu hiyo nchini Congo.

Chanzo: Mwanaspoti