Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CAF watangaza tarehe ya kupanga michezo ya Robo Failnali

A53C623C 95A4 449E A78A 71F0BEE1D189.jpeg CAF watangaza tarehe ya kupanga michezo ya Robo Failnali

Thu, 30 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Mpira Barani Afrika CAF limetangaza kuwa Droo ya Robo Fainali ya CAF Msimu wa 2022/2023 ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho itafanyika Jumatano, 05 Aprili 2023 huko Cairo, Misri.

Michezo ya kukamilisha hatua ya Makundi inafanyika mwishoni mwa juma hili kupata timu nane zitakazosonga kwa hatua inayofuata.

Tanzania inawakilishwa na vilabu viwili, ambapo Simba tayari wameshakata tiketi ya kutinga hatua ya Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika, huku Yanga wakitinga hatua ya Robo Fainali Kombe la Shirikisho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live