Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CAF wamekoshwa na balaa la Kiba

Ali Kiba AFL CAF wamekoshwa na balaa la Kiba

Fri, 20 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chukua hii, sherehe za ufunguzi ‘opening ceremony’ wa mashindano ya African Football League zilizopangwa kufanyika kabla ya mchezo wa Simba vs Al Ahly hazitazidi dakika 10 licha ya maandalizi na uwekezaji wake kuwa mkubwa!

Sherehe hizo ambazo zitakuwa ni kusherekea utamaduni wa Tanzania na Afrika kwa ujumla zitajumuisha ngoma za asili za Tanzania pamoja na performance ya King Kiba.

Performance ya Ally Kiba @officialalikiba leo haitakuwa zaidi ya wimbo mmoja na haitazidi hata dakika tatu!

Inaelezwa kuwa, Kiba hajapata mchongo wa ku-perform kwenye mechi ya ufunguzi wa AFL kwa kuteuliwa bali alituma maombi na kazi zake kama walivyofanya wasanii wengine wa ndani na nje ya nchi.

Kiba ametoboa kwenye dili hilo baada ya waandaaji wa tukio hilo kuvutiwa na performance aliyoifanya kwenye Simba Day ya mwaka huu.

Unaambiwa kampuni ambayo imepewa jukumu la kusimamia opening ceremony Black Engineering imeshafanya kazi na FIFA pamoja na CAF kwenye matukio yao mengi makubwa.

Black Engineering ni wataalam wa matukio kama hayo, wameshafanya kwenye matukio mengi makubwa duniani kama Kombe la Dunia, Olympic, UEFA Champions League n.k.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live