Shirikisho la Soka barani la Afrika CAF limetoa waraka rasmi wa maandishi ikilaani kauli ya rais wa klabu ya Napoli Aurelio De Laurentiis aliyoitoa dhidi ya wachezaji wa afrika na kutaka shirikisho la soka barani ulaya UEFA kumchukulia hatua za kinadhamu kwa kitendo hicho.
Aurelio De Laurentiis alitoa kauli hiyo kwenye hafla ambayo ilikuwa ikioneshwa mubashara ambapo alikuwa akilalamika na kusema kuwa hataki tena kumsajili mchezaji yoyote kutoka Afrika isipokuwa atamuhakikishia kwa maandishi kuwa hatashiriki michuano ya mataifa hiru afrika.
“CAF imeshtushwa na kauli ya kibaguzi isiyo kubalika iliyotolewa na raisi wa klabu ya Napoli Mr Aurelio De Laurentiis kwa wachezaji wa Afrika na mashindano ya mataifa huru Afrika,” waraka rasmi ulisomeka
CAF kwenye waraka wake wameuomba UEFA imchukulie hatua stahiki raisi huyo wa klabu ya Napoli kwa sababu amevunja sheria za UEFA kifungu cha 14, kwa kutoa kazi kwa kigezo cha shinikizo.