Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bwalya awindwa akaungane na Pablo

Bwalya Pic Data Kiungo wa Simba SC, Rally Bwalya

Wed, 1 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taarifa za ndani zinasema kuwa kiungo wa Simba, Rally Bwalya ameshamwaga wino wa kujiunga na klabu ya Amazulu ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini, lakini uongozi wa Wekundu wa Msimbazi umesema umepokea ofa ya mchezaji huyo na utakaa na klabu hiyo ya Sauzi kuona kama dili ni zuri imuuze kwa sababu bado ana mkataba wa mwaka mmoja.

“Kwenye barua yao, Amazulu wameeleza wako tayari kumpa ofa nono Bwalya na wapo tayari kutoa pesa ndefu ili kumsajili, itabidi tukae nao chini ili kuona namna gani kama tunaweza kukubaliana ili kuwapa mchezaji au kama itashindikana watamuacha mchezaji wetu,” kilisema chanzo chetu cha ndani.

Mwaka 2020 Simba ilimsajili Bwalya kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Power Dynamos ya Ligi Kuu Zambia ametumikia mkataba huo kwa miaka miwili na mwisho wa msimu ujao ndio unamalizika.

Alipotafutwa Bwalya alisema mara zote mchezaji mzuri lazima atazivutia timu nyingi mbalimbali na hilo alikuwa anakutana nalo tangu akiwa Zambia kabla ya kujiunga na Simba.

“Bado nina mkataba Simba hao Amazulu wanatakiwa kuzungumza na viongozi wangu kwa sasa sina ruhusa ya kuongea ila kama watamalizana wao huko ndio litakuja kwangu nitaona uamuzi wangu ni upi,” alisema Bwalya.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ alithibitisha kupokea ofa ya Bwalya kutoka Amazulu ila bado hawajafanya uamuzi wowote kuhusu suala hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live