Mon, 11 Dec 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Mshambuliaji raia wa Congo DR, Walter Bwalya ameshinda kesi dhidi ya Klabu ya Wydad.
Bwalya aliiripoti iliyokuwa klabu yake ya Wydad AC kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) kwa kukiuka mkataba kinyume cha sheria na kusitishwa,
FIFA iliomba Wydad imlipe USD $680,803.78 kama mshahara pamoja na riba ya ziada ya 5% juu yake au kuhatarisha marufuku nyingine,
Bwayla alisajiliwa Wydad AC kuchukua nafasi ya Bouly Junior Sambou ambaye aliondoka kwenda Saudia lakini alirejea baada ya kushindwa kwake, hivyo Wydad AC wakaamua kumvunjia Bwalya mkataba.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live