Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Buswita: Gari la Namungo limewaka

Pius Buswita.jpeg Buswita: Gari la Namungo limewaka

Wed, 6 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kutupia bao la nne msimu huu wa Ligi Kuu Bara, kiungo mshambuliaji wa Namungo, Pius Buswita ametamba kuwa gari lao limeanza kuchanganya na  hashindani na mtu kwenye upachikaji mabao bali anaipambania timu yake kurudi kimataifa.

Buswita ambaye ni staa wa zamani wa Yanga, Jumapili dhidi ya Dodoma Jiji aliifungia Namungo bao la ushindi katika mchezo wa ligi uliochezwa kwenye Uwanja wa Majaliwa, Lindi.

Akizungumza nasi, Buswita alisema kuwa pamoja na kufunga lakini anachoangalia zaidi ni timu kuvuna pointi nyingi ambazo zitawarudisha tena kimataifa baada ya kushiriki msimu wa 2021/22.

“Pointi tatu ndio muhimu zaidi, idadi ya mabao sio kipaumbele changu kwasasa, malengo yetu kama timu ni kuona tunakuwa miongoni mwa timu nne zitakazoiwakilisha Tanzania kimataifa;

“Tulianza vibaya sasa tunasogea na kuwa timu zenye ushindani hili ndio linaturudisha kwenye ubora wetu wa misimu miwili nyuma naamini tutafikia malengo kama tutaendeleza ushindani huu,” alisema.

Kuhusu mwenendo wa ligi, Buswita alisema ligi ni ngumu na yenye ushindani ila wamejipanga kuhakikisha wanapambania kumaliza nafasi nne za juu. Namungo imepanda hadi nafasi ya nane kutoka nafasi ya 12.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live