Kocha mkuu wa Barcelona Xavi anakubali Sergio Busquets anaweza kuamua kumalizia soka lake la Barcelona kwa kiwango cha juu mwishoni mwa msimu huu, ingawa kocha huyo wa Blaugrana ana matumaini ya kumbakisha kiungo huyo.
Busquets ameshinda mataji 31 makubwa katika kipindi cha miaka 15 akiwa na timu ya wakubwa ya Barca lakini mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 na wababe hao wa Catalan unamalizika mwishoni mwa msimu huu.
Wakati rais wa Barca Joan Laporta alifichua kuwa klabu hiyo ilitaka kumpa Busquets nyongeza ya mwaka mmoja mwezi uliopita, Inter Miami ya MLS kwa muda mrefu imekuwa ikitajwa kumtaka.
Barca wako pointi 12 mbele ya Real Madrid kwenye msimamo wa LaLiga kabla ya kukutana hii leo na Girona na wakati Xavi anatumai Busquets atasalia Camp Nou, anakubali nahodha wake anaweza kuona ushindi wa taji kama wakati mwafaka wa kuondoka.
Xavi amesema; “Wacha tuone jinsi anavyomaliza msimu. Nimesema mara nyingi, kwangu Busquets ni muhimu sana, sio tu katika mpira wa miguu lakini pia kwenye chumba cha kubadilishia nguo. Nimemwambia mara nyingi, nataka abaki lakini pia namuelewa.”
Nimemwambia, ikiwa kila kitu kitaenda sawa, mwaka huu anaweza kuondoka na mataji na kwa wakati mzuri. Ninamuelewa kabisa ni ngumu sana nitasisitiza aendelee kubaki. Alimaliza namna hiyo kocha huyo.