Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Busara za CAF kuamua hatma ya Biashara United Kimataifa

Biashara Araaaa Kikosi cha Biashara United

Mon, 25 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Biashara United, mpaka sasa ipo njia panda kuhusiana na ushiriki wake katika Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Biashara United ilikuwa isafiri kwenda nchini Libya kupambana na Al Ahly Tripoli katika mchezo wa marudiano hatua ya awali Kombe la Shirikisho Afrika.

Katika mchezo wa kwanza uliopigwa katika dimba la Mkapa Jijini Dar es Salaam, Biashara United waliibuka na ushindi wa goli 2-0.

Mchezo wa marudiano ulikuwa upigwe siku ya Jumamosi Oktoba 23, lakini Biashara hawakusafiri.

Shirikisho la Soka nchini, TFF, wakaiandikia barua CAF kuomba mchezo huo usogezwe mbele, na sababu za kushindwa kufika kwa biashara zikaelezwa, lakini siku ya mechi husika mwenyeji ambae ni Al Ahly Tripoli walipeleka timu uwanjani na waamuzi wakamaliza mechi kuashiria mpinzani hajatokea uwanjani.

Baada ya tukio hilo kumekuwa na taarifa zenye mkanganyiko kutoka kila eneo kuna wanaosema klabu ya Biashara imeondolewa mashindanoni na kupewa adhabu ya kulipa faini na CAF.

TFF katika taarifa yake wanasema bado CAF haijawapa majibu kama wamekubali ama ombi lao limekataliwa.

Droo ya kupanga makundi inapangwa kesho siku ya Jumanne pengine Watanzania watapata kufahamu upi hasa uamuzi wa CAF katika suala hilo la Biashara United.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live