Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Burundi kutumia dimba la Mkapa kufuzu AFCON

Kwa Mkapa Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam

Fri, 13 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya taifa ya Burundi 'The Swallows' watakuwa wenyeji wa Cameroon katika mchezo wa Kundi C wa kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2023 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Alexandre Muyenge, Rais wa Shirikisho la Soka la Burundi alithibitisha kwa Cecafa kwamba watatumia Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dare es salaam kama uwanja wao wa nyumbani.

“Kwa kuwa hakuna Uwanja wetu hata mmoja ulioidhinishwa na CAF, tumeamua kuutumia Uwanja wa Tanzania kama uwanja wa nyumbani kwa mechi zetu za kufuzu AFCON 2023,” alisema Muyenge.

Baada ya kucheza mchezo wao wa kwanza wa Kundi C kwa kuwafuata Namibia nyumbani kwao, baadae tarehe 4 mwezi Juni The Swallows watakuwa wenyeji wa Indomitable Lions ya Cameroon siku nne baadaye jijini Dar es Salaam.Wanachama wengine wa CECAFA ambao hawatatumia Viwanja vyao vya nyumbani kwa sababu havijaruhusiwa na CAF ni pamoja na Sudan Kusini na Ethiopia.

Sudan Kusini itatumia Uwanja wa St. Marys Kitende wa nchini Uganda kuwa uwanja wao wa nyumbani, huku Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka la Ethiopia (EFF), Bahiru Tilahun Limenih akisema watacheza michezo yao ya nyumbani kati ya nchi za Malawi au Afrika Kusini.

Shirikisho la Soka la Rwanda (FERWAFA) pia linasubiri kuidhinishiwa Uwanja na CAF. Timu za CECAFA zitakazochuana kuwania kufuzu AFCON 2023 ni pamoja na Sudan, Ethiopia, Uganda, Rwanda, Burundi, Sudan Kusini, Kenya na Tanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live