Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bunge SC yaibugiza Sudan bao 2-1

Bunge Stars Bunge SC yaibugiza Sudan bao 2-1

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bunge SC -Soka maarufu kama Tulia Boys wameendelea kung’ara katika Michezo ya 13 ya Mabunge ya Afrika Mashariki hapa Kigali Rwanda baada ya kuwalaza Sudan Kusini mabao 2-1 katika mchezo mkali na wenye matumizi makubwa ya nguvu.

Haikuwa kazi rahis kwa Bunge SC -Soka hasa kutokana na kukabiliana na wachezaji warefu na wenye miili mikubwa na ambao kwao Matumizi ya nguvu ndo kila kitu .

Pamoja na matumizi ya nguvu ya wapinzani, Bunge SC ilienda mapumziko ikiongoza kwa bao lililofungwa na Festo Sanga Senator (Makete) kufuatia pasi ya Nahodha Cosato Chumi (Mafinga Mjini).

Mlinda mlango wa Bunge SC Abubakar Asenga (Ifakara) aliibuka shujaa kufuatia kucheza kwa uhodari mkubwa penati waliyopata Sudan Kusini.

Kipindi Cha pili Sudan walisawazisha kufuatia mpira wa adhabu iliopigwa na Lomolo George.

Zikiwa zimesalia dakika tano mchezo kumalizika Simai Hassan ( Nungwi) aliitendea haki pasi mpenyezo ya Jafary Chege ( Rorya) na kuipatia Bunge bao la pili na la Ushindi.

Kwa Ushindi huo, Bunge inaendelea kukaa kileleni ikiwa na point sita, magoli sita ya kufunga na kufungwa magoli mawili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live