Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bundi aendelea kutanda Afrika, Cameroon nayo yaanza kwa kipigo

Embolo Mfungaji wa bao pekee la Uswiss

Thu, 24 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Michuano ya Kombe la Dunia inaingia siku ya tano nchini Qatar ambapo wawakilishi wengine kutoka bara la Afrika timu ya Cameroon imekubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Uswiss.

Mchezo huo wa kundi G, uliopigwa katika uwanja wa Al Janoub umeshuhudia timu ya nne kati ya tano kutoka barani Afrika ikitupa karata yake ya kwanza mbele ya Uswiss.

Katika mchezo huo Cameroon ilioutawala kwa kiasi kikubwa imeshuhudia ikipoteza mbele ya Rais wa Chama cha Sika nchi Cameroon, Samuel Eto'o.

Goli la pekee na la ushindi la Uswiss limefungwa na Breel Embolo ambae ameacha gumzo katika mchezo huo kutokana na kushindwa kushangilia bao hilo na hii ni kutokana na Staa huyo anayekipiga Monaco kuwa mzaliwa wa Cameroon.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live