Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bundesliga: Kuna mtu anapigwa na kitu kizito

Bayern Mapumziko Wachezaji wa Bayern Munich

Sun, 3 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Huko Ujerumani kinachoendelea ni kama ile hadithi ya nani atamfunga paka kengele. Ni raundi ya 24 kwenye Bundesliga huku safari hii ikitegewa FC Cologne kuisimamisha Bayern Leverkusen inayoongoza msimamo wa ligi hiyo, huku ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja.

Juzi Ijumaa raundi hiyo ilifunguliwa kwa mchezo kati ya Bayern Munich dhidi ya pazia la michezo ya raundi ya 24 lilifunguliwa jana, Ijumaa usiku kwa Bayern Munich iliyokuwa ugenini dhidi ya Freiburg na kutoka sare ya mabao 2-2 kwenye Uwanja wa Europa-Park, mabao yaChristian Gunter na Lucas Holer kwa Freiburg na Mathys Tel na Jamal Musiala kwa upande wa Bayern.

Kwa matokeo hayo, Bayern ionasalia nafasi ya pili na pointi 54, huku Freiburg ikiwa nafasi ya tisa kabla ya michezo ya leo na kesho.

Borussia Dortmund na RB Leipzig kila mmoja akiwa ugenini, wanaendelea na vita yao ya kupigania nafasi ya nne, mmoja atakuwa mgeni wa Union Berlin huku mwingine akiwa wa Bochum, wababe hao wamepishana pointi moja tu hivyo mmoja akiteleza anaweza kujikuta akishushwa na mwenzake.

RB Leipzig ambayo itacheza dhidi ya Bochum inalenga kurejea kwenye wimbi lake la ushindi baada ya wikiendi iliyopita kutandikwa nyumbani dhidi ya Bayern Munich kwa mabao 2-1.

Vijana hao wa Marco Rose ambao wapo nafasi ya tano kwenye msimamo wakiwa na pointi 41 wameshinda mechi mbili tu kati ya nane zilizopita (D2, L4) wako katika hatari ya kupoteza nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Mashabiki wa Borussia Dortmund waliishukuru Bayern Munich wikiendi iliyopita kwa kuwapunguza kasi RB Leipzig maana walitandikwa na wao kwa mabao 3-2 wakiwa nyumbani dhidi ya Hoffenheim hivyo walikuwa katika hatari ya kushushwa katika nafasi ya nne waliyopo hivyo kazi kwao leo wakati wakiikabili Union Berlin.

Kwa upande wa FC Cologne ambao wataikaribisha Bayern Leverkusen, wapo kwenye hatari ya kushuka daraja, huku ikikamata nafasi ya 16 kwenye Bundesliga baada ya kujikusanyia pointi 17, katika michezo michache iliyopita, wameonyesha kubadilika, wakitoka sare mara tatu na kushinda mchezo mmoja.

Kazi ipo kwa FC Cologne maana wageni wao kwenye uwanja RheinEnergie wapo kwenye kiwango bora zaidi, ndio timu pekee kwenye zile ligi tano bora barani Ulaya ambayo bado haijapoteza, hii kazi ya kuisimamisha Bayern Leverkusen iliwashinda hadi Bayern Munich na hata Borussia Dortmund.

Miongoni mwa wachezaji hatari kwenye kikosi cha Bayern Leverkusen ambao FC Cologne inapaswa kuwa nao macho ni pamoja na Florian Wirtz amekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi hicho, fundi huyo ni miongoni mwa wachezaji wenye asisti nyingi zaidi kwenye ligi tano bora Ulaya. Ametoa asisti 10 na kupachika mabao manne.

Takwimu zinaonyesha timu hizo zimekutana mara 21, Bayern Leverkusen imeshinda mara 10 huku Cologne naye akishinda mara saba, wametoka sare kwenye michezo minne.

Mechi kali

FC Cologne (4-2-3-1): Schwäbe; Carstensen, Kilian, Chabot, Finkgrafe; Martel, Huseinbasic; Ljubicic, Kainz, Diehl, Thielmann.

Bayer Leverkusen (3-5-2): Hradecky; Kossounou, Tah, Tapsoba; Frimpong, Andrich, Xhaka, Grimaldo; Wirtz, Asli, Schick

Chanzo: Mwanaspoti