Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Buku tano tu kuiona Simba, Power Dynamos

69532 Buku+tano+simba+picha

Sat, 3 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

KOCHA wa Simba, Patrick Aussems amesema wadau na mashabiki wa timu hiyo wajiandae kupokea burudani ya kikosi chao, uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam  katika kilele cha wiki ya Simba, Agosti 6 mbele ya Power Dynamos.

Aussems alisema hayo, walipokuwa wakifanya ziara ya kuwatembelea wadhamini wao wakuu,  Sportpesa ambao waliwapa nguvu ya kufanya vizuri msimi uliopita.

Mbelgiji huyo, alisema kama ilivyokuwa msimu uliopita, mashabiki na wadau watapata nafasi ya kutambulishwa wachezaji wao ambao wataenda kuwatumikia msimu ujao.

"Tulikuwa na msimu mzuri, mategemeo ya kila mmoja wetu ni kufanya vizuri zaidi hilo lipo wazi,  washabiki wetu walifanya kazi kubwa ya kuwa nyuma yetu hasa katika michezo ya Ligi ya Mabingwa.

"Nitatoa nafasi ya kucheza kwa karibu kila mchezaji kwa sababu mchezo ambao tutacheza wa kirafiki ni sehemu ya maandalizi ya msimu ujao, " alisema kocha huyo.

Viingilio ambavyo vimewekwa kwenye tamasha la Simba Day,  mzunguko ni 5,000, VIP A na B,  15000,VIP A 30, 000 huku Platinum ya kawaida  ikiwa 100,000 na Platinum plus,150,000.

Pia alisema kati ya malengo yao makuu ambayo msimu ujao wanahitaji kuyafikia ni kutetea tena ubingwa wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na kuvuka robo fainali ya Ligi ya Mabingwa  Afrika.

"Nina kikosi kizuri chenye wachezaji ambao wanaweza kufanya lolote, nawajibika pia kuimarisha viwango vya wachezaji wangu, " alisema Mbelgiji.

Chanzo: mwananchi.co.tz