Mshambuliaji wa Arsenal Bukayo Saka amefunga mabao 3 (Hat trick) kwa mara ya kwanza kwenye maisha yake ya soka na amekuwa mchezaji wa kwanza mwenye umri mdogo akiwa na miaka 21 na siku 287 anaetoka katika klabu ya Arsenal kufunga Hat trick kwenye timu ya taifa ya England tangu mwa 2008 alipofanya hivyo Theo Walcott.
Saka ameweka rekodi hiyo usiku wa kuamkia leo baada ya kufunga mabao 3 kwenye mchezo dhidi ya North Mecedonia mchezo ambao England imeshinda mabao 7-0, mchezo wa kundi C wa kuwania kufuzu fainali za michuano ya mataifa barani Ulaya Euro 2024. Saka alifunga mabao yake dakika ya 38, 47 na 51.
Upande mwingione Kylian Mbappe amekuwa mchezaji wa 5 kwenye timu ya taifa ya Ufaransa kufunga mabao 40. Mbappe amefikia idadi hiyo ya mabao baada ya kufunga bao la pekee kwenye ushindi wa bao 1-0 walioupata Ufaransa dhidi ya Ugiriki.
Mbappe anaungana na Oliver Giroud mwenye mabao 54, Thierry Henry mabao 51, Antonine Griezmann 43 na Michel Platini mabao 41. Mshambuliaji huyo wa PSG amefikisha mabao 54 kwenye kalenda ya msimu 2022-23 akiwa ni mchezaji wa kwanza raia wa ufaransa kufikia idadi hiyo.