Arsenal wanaripotiwa kuwa na matumaini ya kumsainisha Bukayo Saka mkataba mpya wa miaka sita hadi msimu wa joto wa 2027.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza anaendelea kuimarika chini ya ukufunzi wa Mikel Arteta, akiwa amepata mabao manne na asisti nne katika mechi 20 za michuano yote msimu huu.
Bukayo Saka alisaini mkataba mpya na klabu hiyo mwaka jana, huku masharti yake ya sasa yakimbakiza hadi mwisho wa kampeni ya 2023-24.
Hata hivyo, mwanahabari Ekrem Konur anadai kwamba Arsenal sasa wamedhamiria kujihakikishia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 anasalia kwa muda mrefu zaidi, kwa ofa ya mkataba hadi 2027.
Mkataba kama huo ungemfanya Bukayo Saka kusalia katika klabu hiyo baada ya kutimiza umri wa miaka 25, huku mshambuliaji huyo akiwa tayari ameshafunga mabao 15 na asisti 25 kwenye michezo 108 aliyoichezea klabu yake ya utotoni.