Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bukayo Saka kusaini Mkataba mpya Arsenal

Bukayo Saka New Contract Bukayo Saka

Sat, 25 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Winga wa kimataifa wa England Bukayo Saka yuko mbioni kumwaga wino wa kuendelea kukitumikia kikosi cha Washika Mtutu wa London, Arsenal.

Saka, 21, akiwa mmoja kati ya wale wachezaji muhimu kwenye kikosi cha kocha Mikel Arteta amekuwa na mazungumzo ya mkataba mpya na waajiri wake kufuatia kandarasi iliyokuwepo sasa kufikia tamati mwaka 2024.

Msimu huu Saka ambaye alianza kuichezea The gunners mwaka 2018 amefunga magoli tisa na kutoa assisti bao nane kwenye jumla ya mechi 23 alizocheza msimu huu za Arsenal.

Mkataba mpya unatajwa kuwa utafikia tamati 2028 ambapo utakuwa na thamani ya pauni milioni 10 kwa mwaka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live