Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bukayo Saka atoa kauli hatma yake Arsenal

Bukayo Saka New Nyota wa Arsenal, Bukayo Saka

Sat, 25 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Habari ndo hiyo. Bukayo Sake amewaambia mabosi wa Arsenal kuwa anataka kubaki kwenye kikosi hicho cha Emirates.

Na sasa winga huyo wa England yupo kwenye mazungumzo ya mkataba mpya utakaomshuhudia akilipwa Pauni 200,000 kwa wiki. Saka amekuwa kwenye kiwango bora tangu alipotoka kwenye fainali za Kombe la Dunia 2022 huko Qatar.

Saka, 21, alitajwa kwenye kikosi cha michuano hiyo cha L'Equipe na kuonyesha jinsi alivyo na ubora mkubwa ndani ya uwanja. Kiwango chake bora cha uwanjani kiliibua wasiwasi kama mchezaji huyo angeendelea kubaki kwenye kikosi cha Arsenal.

Ripoti za sasa zinadai kwamba mchezaji huyo ameshafikia makubaliano ya awali ya kuongeza mkataba mpya.

Hata hivyo, jambo hilo bado halijamalika na litachukua muda, lakini mchezaji mwenyewe ameweka wazi anahitaji kubaki kuendelea kuwapo kwenye kikosi hicho cha kocha Mikel Arteta. Daily Mail linadai kwamba Saka amwaambia Arsenal anataka kubaki, huku dili hilo mpya litamfanya aweke kibindoni Pauni 10 milioni kwa mwaka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live