Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bruno avunja ukimya kutua Bayern Munich

Bruno Fernandes Capt Bruno Fernandes

Thu, 16 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nahodha wa Manchester United Bruno Fernandes amethibitisha kuwa atasalia ndani ya klabu hiyo, hataondoka mwishoni mwa msimu huu kama ambavyo imekuwa ikiripotiwa siku za karibuni.

Bruno ameweka wazi juu ya hatma yake ndani ya United, jana usiku baada ya mchezo wa Ligi kuu Englan dhidi ya Newcastle United mchezo ambao Manchester United iliibuka na ushindi wa bao 3-2 katika dimba la Old Traford.

"Nitakuwa hapa. Klabu inanihitaji, klabu inataka niwe sehemu ya mpango ujao wa timu hivyo kama nilivyosema siku zote, sitaki kuwa mchezaji ambaye klabu haitaki kuwa naye na nataka kuwa mchezaji ambaye klabu inanihitaji.” Amesema Bruno Fernandez

Kiungo huyo mshambuliaji raia wa Ureno mwenye umri wa miaka 29 amekuwa akihusishwa kujiunga na vilabu vya Bayern Munich ya Ujerumani, Inter Milan ya Italia na Al Nassr ya Saudi Arabia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live