Nahodha wa klabu ya Manchester United Bruno Fernandes ameomba kama itawezekana kusiwe na kadi ya njano pale ambapo mchezaji atashangilia goli kwa kuvua jezi yake.
“Nafikiri ni moja ya sheria ambazo zinapaswa kubadilishwa, kwasababu utaweza kushangilia goli kwa kuheshimu klabu nyingine na kuufurahia wakati huo.” – Bruno Fernandes.
Maneno hayo aliyazungumza baada ya nyota wa Manchester United Amad Diallo kuonyeshwa kadi ya pili ya njano ya mchezo baada ya kuvua jezi akishangilia alipofungo goli la ushindi la United dakika za mwisho dhidi ya Liverpool.
Manchester United imefuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hii mikubwa kwa kumuondosha Liverpool kwa jumla ya magoli 4-3 baada ya dakika za nyongeza.