Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bruno afunguka alichomwambia tajiri

ASQADWE Bruno afunguka alichomwambia tajiri

Fri, 22 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kukutana na tajiri mpya wa Manchester United, Sir Jim Ratcliffe, kapteni wa timu hiyo, Bruno Fernandes amemwambia kigogo huyo kwamba anahitaji kuendelea kubaki Old Trafford na kuisaidia timu katika kipindi hiki cha kuijenga.

Bruno ambaye ana umri wa miaka, 29, ana mkataba wa kusalia Old Trafford hadi mwaka 2026 kukiwa na kipengele cha kuurefusha kwa mwaka mmoja zaidi, katika dirisha lililopita alikuwa akihusishwa kuondoka huku ripoti zikidai alitengewa zaidi ya Pauni 80 milioni kwa mwaka na matajiri wa Saudi Arabia.

“Nimeshakutana na mmiliki mpya, walikuwa wanahitaji kukutana na wachezaji na tayari wameshafanya hivyo, kitu nilichomwambia ni kwamba nataka kubaki hapa, nataka niwe sehemu ya mpango wa kuitengeneza Man United mpya.”

“Naamini mipango yetu ina kila kitu kitakachotuwezesha kupambana na Manchester City, Arsenal na Liverpool, ambazo tayari zimeshakaa vizuri, nahitaji kushindana nao na kushinda.”

Alisema Fernandes na kusisitiza kwamba hana matumaini kwamba Man United inaweza kuchukuwa taji mapema kutokana na hali yao.

“Sitaki kuwaahidi kwamba tunakwenda kuwa mabingwa, nafahamu kwamba msimu huu tumekuwa kwenye hali mbaya na hilo sio jambo la kuficha. Ila tunaweza kujipanga.”

Chanzo: Mwanaspoti