Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bruno aanza tambo Singida

Bruno Barroso Tanga Kiungo wa Singida FG, Bruno Gomes

Sun, 18 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Nyota wa Singida Fountain Gate, Bruno Gomes amesema anaanza kurudisha kiwango taratibu baada ya kutokuwa na mwanzo mzuri msimu huu kutokana na kukosa muda mwingi wa kucheza na majeraha aliyokuwa nayo, huku kocha Thabo Senong akimmwagia sifa nyingi kiungo huyo mshambuliaji.

Bruno aliyefunga bao la kwanza la Ligi Kuu Bara msimu huu wakati wa mchezo dhidi ya Tanzania Prisons waliopoteza kwa mabao 3-1, Februari 15, alisema anaendelea kujitafuta ingawa kuna matumaini makubwa mbeleni.

“Unapotaka kulinganisha msimu huu na uliopita ni kweli unaona kuna utofauti mkubwa, lakini hiyo ni changamoto nyingine kwangu nayokabiliana nayo kama inayoweza kumkuta yeyote. Sijakata tamaa ndio maana naendelea kupambana,” alisema

Bruno ambaye msimu uliopita alifunga mabao 10 katika Ligi Kuu. Aliongeza kuwa sio kweli kama ujio wa aliyekuwa nyota wa kikosi hicho, Marouf Tchakei aliyetimkia Ihefu ulimnyima nafasi ya kucheza mara kwa mara, bali anaamini ni suala la ushindani na si vinginevyo.

Kwa upande wa kocha mkuu wa timu hiyo, Thabo Senong alisema bao hilo alilofunga nyota huyo licha ya kupoteza mbele ya Prisons limerejesha hali yake ya kujiamini, kwani hata benchi la ufundi linapenda kuona akifanya vizuri.

Singida inayocheza Ligi Kuu Bara msimu wa pili baada ya kupanda daraja uliopita, imeanza vibaya mechi za kumaliza duru la kwanza kwa kupoteza zote mbele ya Kagera Sugar na Tanzania Prisons.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: