Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bruno Guimaraes kung’oka kirahisi

Bruno Guimares Newcastle Bruno Guimaraes kung’oka kirahisi

Wed, 17 Jan 2024 Chanzo: Dar24

Imefahamika kuywa Kiungo Bruno Guimaraes ana nafasi kubwa ya kuondoka Newcastle United, kufuatia mkataba wake kuwa na kipengele cha kuondoka klabuni hapo.

Kinachoripotiwa ni kwamba kwa timu itakayohitaji huduma ya kiungo huyo inaweza kulipa Pauni 32 kwa awamu tatu ili kufikia kiwango ambazo kimeorodheshwa kwenye mkataba wake.

Tangu alipoondoka Lyon kwenda St James’ Park katika msimu wa 2021-22, Mbrazili huyo amejipambanua na kuweka jina lake kwenye orodha ya viungo wanaofanya vyema kwenye soka la Ulaya kwa sasa, akiisaidia pia Newcastle United kurejea kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Katika mechi 87 alizochezea Newcastle, Guimaraes amefunga mabao 11 na kuasisti 10, licha ya kupangwa kwenye kiungo ya chini na Kocha Eddie Howe.

Kutokana na kuwindwa na timu za Barcelona, Real Madrid, Paris Saint-Germain, Liverpool na Chelsea, Newcastle ilikubali kumpa mkataba mrefu Guimaraes, Oktoba mwaka jana kuhakikisha anabaki kwenye kikosi chao hadi mwishoni mwa msimu wa 2027-28.

Katika dili hilo jipya, Newcastle iliweka kipengele kinachotaja pesa anayouzwa Guimaraes, karibu Pauni 100 milioni.

Chanzo: Dar24