Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bruno Ferry: Kocha bora wa mezi Ligi Kuu

Dabo Azam 128.png Dabo na Bruno Ferry.

Tue, 2 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Azam FC, Bruno Ferry amechaguliwa kuwa Kocha Bora wa mwezi Machi wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2023/24 akiwashinda kocha wa Yanga, Miguel Gamondi na Kocha wa Mtibwa, Zubeir Katwila.

Bruno aliiongoza Azam kushinda michezo miwili kati ya mitatu iliyocheza na kuendelea kubaki nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu.

Azam iliifunga Yanga mabao 2-1, iliifunga Dodoma Jiji mabao 4-1 kisha ikatoka sare ya bao moja na Coastal Union.

Pia Kamati ya Tuzo imemchagua Meneja wa Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma, Shabani Rajabu, kuwa Meneja Bora wa Uwanja kwa mwezi Machi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live