Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bruno Fernandes Kuwakosa Burnley

Bruno Fernandes Man Utd 1536x864 Kiungo mshambuliaji wa Manchester United, Bruno Fernandes

Wed, 29 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Manchester United italazimika kuingia dimbani bila Bruno Fernandes kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Burnley Alhamisi dimbani Old Trafford.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno alicheza dakika 90 wakati Mashetani Wekundu wakitoka sare ya 1-1 na Newcastle United Jumatatu usiku.

Hata hivyo, kadi ya njano ya Fernandes katika dakika ya 66 ilikuwa onyo lake la tano msimu huu wa ligi, na kwa sababu hiyo atatumikia marufuku ya mechi moja wiki hii.

Mchezaji huyo wa zamani wa Sporting Lisbon alishindwa kucheka na nyavu au asisti katika mechi ya tatu mfululizo za Ligi Kuu ya Uingereza Jumatatu na amerekodi bao moja pekee katika mechi saba za mwisho za ligi kuu.

Sare ya Man United siku ya Jumatatu inawafanya kuwa na pungufu ya pointi saba kwenye nafasi kuelekea nne bora huku wakiwa na mechi mbili mkononi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live