Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Brighton waomba radhi na chama cha waamuzi EPL

PMGOL.jpeg Brighton waomba radhi na chama cha waamuzi EPL

Fri, 21 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamati ya waamuzi wa England, PGMOL, imeiomba radhi klabu ya Brighton & Hove baada ya kunyimwa penati ha wazi dhidi ya Tottenham Hotspur hapo siku Jumamosi.

Matokeo yakiwa 1-1, Brighton & Hove walistahili kupata penati baada ya mchezaji wa Tottenham Hotspur, Pierre-Emile Hojbjerg, kumshika ndani ya eneo la hatari Kaoru Mitoma wa Brighton & Hove.

Lakini mwamuzi Stuart Attwell akapeta kuashiria mchezo uendelee bila kujiridhisha angalau hata kuangalia VAR licha ya wachezaji wa Brighton & Hove kumtaka mwamuzi huyo kufanya hivyo.

Kocha wa Brighton, Roberto De Zerbi, alioneshwa kukerwa na tukio hilo na kumfuata mwamuzi kuzungumza naye kwa hasira.

Sasa Mkuu wa kamati ya waamuzi, Howard Webb, amejitokeza hadharani kwa niaba ya kamati kuwaomba radhi Brighton.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: