Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Brentford yazikomaliza Arsenal, Spurs kwa Toney

Southgate Anadokeza Kuhusu Kuanza Kwa Toney Kwenye Euro 2024 Mshambuliaji wa klabu ya Brentford Ivan Toney

Wed, 19 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Ofa ya Pauni 40 milioni iliyowasilishwa na Tottenham kwenda Brentford kwa ajili ya kumsajili straika wao, Ivan Toney dirisha hili imekataliwa na timu hiyo imeendelea kushikilia msimamo wao kwenye kiasi cha pesa inachokihitaji ili kumuuza mchezaji huyo muhimu ambaye anahitajika na Arsenal pia.

Inaelezwa Brentford inahitaji Pauni 65 milioni ili kumuuza Toney mwenye umri wa miaka 28, lakini wanaweza kukubali ofa inayofikia Pauni 55 milioni.

Spurs inamtaka Toney kwa ajili ya kuweka sawa eneo lao la ushambuliaji baada ya kutofanya vizuri msimu uliopita na imepanga kufanya kila linalowezekana kwa ajili ya kumsajili.

Staa huyu wa kimataifa wa England ambaye pia yupo kwenye rada za Arsenal, anataka kuondoka katika dirisha hili kwa ajili ya kutafuta changamoto mpya sehemu nyingine ili kushinda mataji na kupata mafanikio zaidi.

Arsenal ilimaliza ya pili msimu uliopita na itacheza michuano ya Ligi ya Mabingwa jambo ambalo litamvutia zaidi Toney.

REAL Mallorca imefikia patamu kwenye mazungumzo yao na beki wa Borussia Dortmund na Ujerumani, Mats Hummels, 35, baada ya kuondoka Borussia Dortmund katika dirisha hili. Hummels ambaye pia anawindwa na AS Roma, msimu uliomalizika alicheza mechi 40 za michuano yote, amefikia makubaliano ya kuondoka Dortmund baada ya kukaa katika timu hiyo kwa zaidi ya miaka 16.

WINGA wa Everton Ashley Young, 38, yup kwenye hatua za mwisho kufikia makubaliano na mabosi wa timu hiyo kwa ajili ya kusaini mkataba mpya wa mwaka mmoja utakaomwezesha kusalia katika timu hiyo kwa msimu mmoja zaidi. Young ambaye mkataba wake wa sasa unamalizika mwisho wa mwezi huu, msimu uliopita alicheza mechi 34 za michuano yote.

TOTTENHAM bado haijakata tamaa katika mpango wao wa kutaka kumsajili beki wa kulia wa AS Monaco Vanderson, 22, na inataka kumsajili katika dirisha hili. Msimu uliopita Vanderson amecheza mechi 23 za michuano yote na kufunga mabao matatu. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2028 na mabosi wa Spurs wanataka kuhakikisha nyota huyo anatua klabuni hapo.

STRAIKA wa Aston Villa, Jhon Duran ameweka wazi angependa kujiunga na Chelsea katika dirisha hili na kupambania namba katika kikosi cha kwanza cha matajiri hao wa Jiji la London. Duran anahusishwa kuwa katika rada za mabosi wa Chelsea tangu mwezi uliopita. Mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.

ARSENAL na Chelsea zimeingia vitani dhidi ya AC Milan na Borussia Dortmund ili kuipata saini ya straika wa Stuttgart na Guinea, Serhou Guirassy dirisha hili. Kwa mujibu wa tovuti ya BILD, Serhou katika mkataba wake kuna kipengele kinachomwezesha kuondoka ikiwa timu inayomhitaji italipa kiasi kisichozidi Pauni 30 milioni.

JUVENTUS imeipa Arsenal ofa ya pesa na Arthur Melo ili ikubali kuwauzia beki wao Jakub Kiwior dirisha hili. Kiwior hajapata nafasi kubwa ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Arsenal kwa msimu uliopita ambapo alicheza mechi 31 za michuano yote ambazo nyingi aliingia akitokea benchi. Mkataba wa Kiwior unamalizika mwaka 2028.

NAPOLI imeendelea kusisitiza haina mpango wa kumuuza winga wao raia wa Georgia, Khvicha Kvaratskhelia dirisha hili licha ya wakala wa staa huyo kufunguka mchezaji wake anataka kuondoka kwa ajili ta kutafuta changamoto mpya sehemu nyingine. PSG ni moja kati ya timu zilizotajwa kutaka kumsajili winga huyu ambaye msimu uliopita alifunga mabao.

Chanzo: Mwanaspoti