Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Brentford yapandisha ada ya Ivan Toney

Ivan Toney Mshambuliaji wa klabu ya Brentford Ivan Toney

Thu, 2 Nov 2023 Chanzo: Dar24

Mabosi wa Klabu ya Brentford wanadaiwa kuhitaji Pauni 80 milioni ili kumpiga bei Mshambuliaji wao, Ivan Toney katika dirisha lijalo la majira ya baridi, ambapo vigogo wengi Barani Ulaya wameonyesha nia ya kutaka kumsajili.

Licha ya Mshambuliaji huyu kutocheza tangu kuanza kwa msimu huu, huduma yake imekuwa ikimendewa na vigogo wengi Barani Ulaya ambao wamevutiwa na kiwango alichoonyesha msimu uliopita.

Arsenal ni miongoni mwa timu zinazoonekana kuhitaji sana huduma yake, lakini huenda ikarudi nyuma kutokana na kiasi kikubwa cha pesa kinachohitajika na mabosi hao.

Awali ripoti zilidai kuwa, Klabu ya Brentford ilihitaji Pauni 60 Milioni ili kumuuza Mshambuliaji huyo lakini baada ya kuona kuna timu nyingi zenye uhitaji na Mshambuliaji wao wameonekana kupandisha dau lake.

Toney ambaye ni Mshambuliaji wa kimataifa wa England kwa sasa amefungiwa kucheza soka baada ya kukutwa na haia ya kujihu sisha na masuala ya kubeti, mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2025.

Msimu uliopita staa huyu alikuwa wa moto zaidi, alicheza mechi 35 za michuano yote, akafunga mabao 21 na kutoa asisti tano.

Chanzo: Dar24