Mon, 27 Mar 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Baada ya siku kadhaa za presha na tetesi hatimaye pande mbili baina ya Klabu ya Tottenham na kocha wake, Antonio Conte zimeafikiana kuvunja mkataba na sasa timu itakuwa chini ya uangalizi wa kocha wa muda ambaye ni Cristian Stellini.
Kwa maamuzi hayo Spurs inayoshika nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu ya Uingereza inatafuta kocha wa nne ndani ya miaka miwili.
Kabla ya maamuzi hayo Conte hakuwa na uhusiano mzuri na wachezaji na uongozi wa klabu kutoka na kuwashutumu wachezaji wake akidai hawajitumi na kuelezea sababu kadhaa kwa nini timu haitwai mataji.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: