Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Breaking News: Taarifa rasmi ya Yanga kuhusu kuachana na Kocha Nabi

NABI KOCHA MKUU YANGA FD Kocha Nabi

Tue, 25 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

TAARIFA: Uongozi wa Yanga unapenda kuwataarifu mashabiki na Wanachama wake kuwa Nasreddin Nabi, bado ni kocha mkuu wa timu yetu.

Nabi alijiunga na Yanga April, 2021 na amekuwa na rekodi nzuri ya kuiongoza timu yetu kubeba Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita, bila kupoteza.

Akizungumza na YANGA MEDIA, Mtendaji Mkuu wa Yanga, Andre Mtine amewaomba mashabiki na wanachama wa Yanga kufuatilia taarifa za uhakika za timu yao kupitia vyanzo rasmi vya habari vya klabu.

“Niwaombe mashabiki na wanachama wetu kuwa na utaratibu wa kufatilia taarifa za klabu yetu kutoka kwenye vyanzo vyetu vya habari.

“Tuna YANGA APP. Tuna Website ya Young Africans na kurasa zetu za mitandao ya kijamii ambazo zimekuwa zikitoa taarifa za klabu yetu na kwa wakati sahihi,” alisema Andre.

Uongozi unamtakia kila la kheri kocha Nabi na benchi lake la ufundi kwenye maandalizi ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu dhidi ya KMC utakaopigwa saa 1:00 jioni kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live