Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Breaking News: Simba Waachana na Kocha Hitimana

Hitimana Sokalabongo Breaking News: Simba Waachana na Kocha Hitimana

Tue, 28 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha msaidizi wa Simba, Hitimana Thiery amefikia makuliano ya kuachana na timu hiyo.

Kocha huyo alijiunga na Simba kwa ajili ya kuweza kuiongoza katika mashindano ya kimataifa kutokana na aliyekuwa kocha wa wakati huo Didier Gomes kutokidhi vigezo vya CAF.

Kwa sasa timu ya Simba ipo chini ya Kocha Mkuu Pablo Franco mwenye ruhusa ya kukaa kwenye mechi za ushindani za kimataifa akiwa ameweza kuiongoza timu hiyo kwenye mechi za Kombe la Shirikisho.

Amefanikiwa kupenya na timu hiyo mpaka kwenye hatua ya makundi ambapo leo Desemba 28 makundi yamepangwa na timu ya Simba ipo kundi D ikiwa pamoja na timu ya RS Berkane ambapo mchezaji wa zamani wa Simba, Clatous Chama anacheza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live