Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Breaking: Manara afungiwa miaka miwili

MANARA 35454657 1 Haji Manara

Thu, 21 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamati ya Maadili ya TFF imemhukumu Ndugu Haji Manara kutojihusisha na masuala ya soka ndani na nje ya nchi kipindi cha miaka miwili (2) na kutozwa faini ya Tsh. Milioni 20 [Tsh 20,000,000]. Adhabu hiyo inaanza leo Alhamisi, Julai 21, 2022.

Manara alikuwa akituhumiwa kwa kosa la kuwakashifu viongozi wa TFF, kuwatolea maneno ya hovyo na kukiuka kanuni za maadili za Shirikisho la Soka Tanzania.

Katika video iliyosambaa siku ya mechi ya Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam, kati ya Yanga na Coastal Union katika Dimba la Sheikh Amri Abid jijini Arusha, Manara alionekana akirushiana maneno na Rais wa TFF, Wallace Karia hivyo kuitwa mbele ya kamati hiyo kujibu tuhuma ambazo zimemtia kitanzini hii leo.

Ikumbukwe kuwa, si mara ya kwanza kwa Manara kufungiwa, mwaka 2017 akiwa Ofisa Habari wa Simba SC, Manara amlifungiwa kutojihusisha na shughuli za mpira ndani na nje ya nchi kwa muda wa miezi 12 na faini ya shilingi milioni 9, vyote kwa pamoja kwa makosa kama hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live