Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#Breaking: Kocha Goran apewa 'thank you' Tabora United

Gn Taboraaa Kocha Goran apewa 'thank you' Tabora United

Thu, 21 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Klabu ya Tabora United imefikia makubaliano ya pande zote mbili ya kusitisha mkataba na aliyekuwa kocha mkuu Goran Kopunovic, raia wa Serbia kuanzia leo Machi 21.

Tabora United imefikia uamuzi huo kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa matokeo ambayo timu hiyo imekuwa ikiyapata katika michezo yake ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Goran alijiunga na Tabora United Agosti mwaka jana kama kocha mkuu kwa mkataba wa mwaka mmoja ambao ulikuwa umalizike mwishoni mwa msimu huu kabla ya kufikia uamuzi wa kuvunjwa mapema leo hii.

“Tabora United inamshukuru kocha Goran kwa utumishi wake tangu alipojiunga na timu na hivyo inamtakia kila la heri huko aendako,” ilisomeka taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari ya Tabora United, Christina Mwagala.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live