Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Breaking: Heritier Makambo afungasha virago Yanga

Makamboo Heritier Makambo

Sun, 15 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Yanga raia wa Vongo DR, Heritier Ebenezer Makambo ameaga mashabiki wa Yanga baada ya makubaliano na uongozi ya kuvunja mkataba wake.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Yanga, mkataba wa Makambo ulibaki miezi sita, ameondoka klabuni baada ya makubaliano ya pande zote mbili.

Akizungumza na YANGA MEDIA, Makambo amewashukuru mashabiki wa Yanga kwa upendo wao kwake na kuiombea kheri timu iweze kufanya vyema kwenye mashindano wanayoshiriki msimu huu.

"Nawashukuru mashabiki wote kwa sapoti yenu kipindi chote nikiwa hapa, nawatakia kila kheri wachezaji wangu na kuwaombea waweze kufanikiwa kwenye mashindano wanayocheza msimu huu," alisema Makambo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live