Mchezaji kandanda wa Ghana Christian Atsu amethibitishwa kufariki dunia baada ya wiki mbili chini ya kifusi nchini Uturuki baada ya kutokea kwa tetemeko la Ardhi.
Atsu mwenye umri wa miaka 31 aliripotiwa kupatikana saa chache baada ya tukio hilo la kusikitisha lakini ripoti baadaye zilionyesha kuwa ni utambulisho wa makosa.
Kutokana na hali hiyo baadhi ya wanafamilia yake na wakala wake Nana Sekyere walitimkia Uturuki kuungana na klabu yake kumsaka.
Wakati wa utafutaji wa hivi karibuni, viatu vya Atsu vilikuwa vya kwanza kati ya mali nyingine kupatikana.
Baadaye, timu ya utafutaji na uokoaji ilipata hati yake ya kusafiria na vitu vingine ambavyo vilithibitishwa na wakala wake.
Atsu alianza maisha yake ya soka ya kulipwa nchini Ghana kabla ya kuhamia Ulaya kuichezea FC Porto ya Ureno. Kisha alikuwa na vilabu vingine kadhaa, vikiwemo Everton, Bournemouth, na Newcastle United, kabla ya kujiunga na Hatayspor mnamo 2022.