Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Breaking: Aziz Ki na Chama wafungiwa na TFF

Chama Aziz Chama na Aziz Ki

Tue, 8 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wachezaji wa Kimataifa Aziz Ki wa Yanga na Clatous Chama wa Simba wamefungiwa michezo mitatu (3) na kutozwa faini ya Sh. 500,000 (laki tano) kwa kosa la kukwepa kusalimiana na wachezaji wa timu pinzani kabla ya kuanza kwa mchezo wa Yanga dhidi Simba.

Aziz Ki raia wa Bukrina Faso na Chama raia wa Zambia kwa nyakati na mazingira tofauti walionekana kusubiri nje ya uwanja ili kusubiri zoezi la kusalimiana likamilike ndipo waingie kiwanjani.

Adhabu hii ni kwa uzingativu wa Kanuni 41:5(5.4) ya Ligi Kuu kuhusu udhibiti kwa Wachezaji.

Mechi tatu atakazokosa Aziz Ki ni kati ya Yanga dhidi ya; Kagera Sugar, Singida Big Stars, Dodoma Jiji Fc.

Mechi tatu atakazokosa Chama ni kati ya Simba na; Singida Big Stars, Ihefu Sc, Namungo Fc.

Singida Big Stars watazikabili Simba na Yanga bila Chama na KI.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live