Timu ya Brazil ina kila sababu ya kufuzu kwa michuano ya Kombe la Dunia kule Qatar 2022, baada ya Alfajiri ya leo kuibuka na ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya Uruguay kwa upande wa Bara la Amerika ya Kusini.
Ushindi huo unawafanya Brazil kuweka mwanya wa alama 6 baina yao na anaekamata nafasi ya pili timu ya Argentina.
Ushindi huo umewafanya Brazil kufikisha alama 31 baada ta michezo 11, huku wakiwa wameshinda michezo 10 na kutoa sare mchezo mmoja.
Magoli ya Brazil katika mchezo huo yamefungwa na winga wa Leeds United Raphinha aliefunga magoli mawili, Neymar na Barbosa Almeida huku lile la Uruguay likifungwa na Luis Suarez.
Katika mechi nyingine za Bara la Amerika ya Kusini, Argentina imeshinda goli 1-0 dhidi ya Peru na Chile ikishinda 3-0 dhidi ya Venezuela