Brazil imemtema kikosini winga wa Manchester United Antony kufuatia madai unyanyasaji yaliyotolewa na mpenzi wake wa zamani.
Shirikisho la kandanda la Brazil lilisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 ameondolewa kwenye kikosi baada ya "mambo kujulikana" ambayo "yanahitaji kuchunguzwa".
Chombo cha habari cha Brazil UOL kilichapisha mada yaliyotolewa na mpenzi wa zamani wa Antony siku ya Jumatatu.
Polisi mjini Sao Paulo na Greater Manchester wanachunguza madai hayo, ambayo mchezaji huyo ameyakanusha.
"Ninaweza kusema kwa utulivu kwamba shutuma hizo ni za uongo na kwamba ushahidi uliotolewa tayari na ushahidi mwingine utakaotolewa unaonyesha kwamba sina hatia kwa tuhuma hizo," Antony alisema kwenye mtandao wa kijamii.
"Nina imani kuwa uchunguzi unaoendelea wa polisi utadhihirisha ukweli kuhusu kutokuwa na hatia."
Antony anashutumiwa kwa kumshambulia mpenzi wake wa zamani Gabriela Cavallin "kwa kumpiga kwa kichwa" kwenye chumba cha hoteli mjini Manchester mnamo Januari 15, na kumwacha akiwa amekatwa kichwa ambacho kilihitaji matibabu kutoka kwa daktari.